Friday, April 25, 2014

BUSOKELO, NHC KUJENGA NYUMBA 14 ZA WATUMISHI


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo, Meckson Mwakipunda, alisema mpango huo wa ujenzi wa makazi ya watendaji ni sehemu ya miradi ya kipaumbele katika halmashauri hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba, Martin Mdoe, alisema mradi wa makazi Busokelo ni sehemu ya mkakati wa miaka mitano wa shirika hilo kujenga nyumba za gharama nafuu za madaraja tofauti touti katika maeneo mbalimbali nchini, zikiwemo halmashauri.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo

Baadhi ya watumishi wa shirika la nyumba wakimsikiliza mwenyekiti huyo








HALMASHAURI ya Busokelo katika Wilaya ya Rungwe na Shirika la nyumba (NHC) wameingia kwenye makubaliano ya msingi ya kujenga nyumba 14 kwa ajili ya watumishi wake.

Uamuzi wa kujenga nyumba hizo  unalenga kuboresha utendaji na ufanisi wa halmashauri hiyo  mpya iliyoanzishwa 2012, huku ikiwa inakabiliwa na tatizo kubwa la miundombinu, ikiwemo nyumba za watumishi.

Akizungumza na waandhishi wa habari Jijini hapa, ikiwa ni muda mfupi baada ya kumalizika kikao cha pamoja na watendaji wa shirika la nyumba, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Meckson Mwakipunda, alisema mpango huo wa ujenzi wa makazi ya watendaji ni sehemu ya miradi ya kipaombele katika halmashauri hiyo.

“Kama mnavyojua Busokelo ni halmashuri mpya ambayo ilianza rasmi Oktoba 10 mwaka 2012, na upya huo inachangamoto nyingi hasa makazi ya watumishi na kwenye bajeti yetu ya kwanza ambayo ndio tunaendelea nayo tuliingiza hilo la kujenga nyumba lengo likiwa ni  kuwajali wafanyakazi kwa kuwapa mazi bora ” .

Alisema halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mradi wa kuboresha makazi, ambao umegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza ikiwa ni kujenga nyumba 14 za watumishi, huku awamu ya pili ikihusisha nyumba 36 kati ya  50 zitakazuhusisha miradi hiyo, ambapo baadhi ya nyumba hizo zitauzwa na kupangishwa kwa wananchi wa kawaida.

Alisema serikali kwa kutambua changamoto  ilikubali kuthibitisha bajeti hizo na tayari fedha hizo zimeshaingizwa katika halmashauri hiyo na kilichobaki ni kukamisha hatua za kisheria kati yake na mkandarasi ambaye ni shirika la nyumba ambalo litahusika katika ujenzi huo.

Akizungumzia muda wa kuanza kwa mradi huo, Mwakipunda alisema kinachosubiliwa hivi sasa ni halmashauri hiyo kupata Baraka za Wizara ya Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuidhinisha vibali vya miradi ya aina hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba, Martin Mdoe, alisema mradi wa makazi Busokelo ni sehemu ya mkakati wa miaka mitano wa shirika hilo kujenga nyumba za gharama nafuu za madaraja tofauti touti katika maeneo mbalimbali nchini, zikiwemo halmashauri.

“Kipaumbele cha mkakati huu ni kwa halmashauri mpya 16 nchini, ambazo katika maeneo yao hakuna nyumba za kutosha , miongoni mwa halmashauri hizo katika mkoa wa Mbeya tumeanza na Halmashauri ya Busokelo”
Mwisho.

Mbeya yetu blog

No comments: