Wakati Jitihada zikifanyika Kurudisha mMawasiliano ya Barabara, Makamanda Wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Wakitafakari Juu ya Kuweka Daraja la Muda

 Mawasiliano kati ya Dar na Bagamoyo kwa barabara ya Bagamoyo yamekatika. Maji yanayopita katika mto Mpigi ambako daraja halipitiki ni mengi sana kiasi kwamba nguzo tatu zinazopitisha umeme mkubwa kwenda Bagamoyo zipo hatarini. Mojawapo maji yanaikaribia zaidi na uwezekano wa kusombwa ni mkubwa kwa sababu miti mikubwa iliyokuwa karibu na eneo hilo nayo imeng'olewa kirahisi kabisa. 
Wakati jitihada zikifanyika kurudisha mawasiliano ya barabara na makamanda wakitafakari juu ya kuweka daraja la muda, watu wameanza lawama eti mkandarasi. Lakini ukweli ni mambo ni matatizo yetu wenyewe. Ukiangalia kati ya hizi picha, kuna moja inaonekana na matete katikati na pembeni yake, kushoto na kulia yanapita maji. Maeneo haya yanayopita maji kwa kipindi fulani yalikuwa yakichimbwa mchanga na kuacha katikati ya mto kuwa na mwinuko. Mvua nyingi maji yamepita pembeni na hata kwenda nje ya daraja.Picha zote na Mdau - Abel Ngapemba

Comments