VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA VYAENDELEA NA MAZOEZI KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MUUNGANO APRILI 26 KWENYE UWANJA WA UHURU
Vikosi vua ulinzi na usalama vikiwa katika mazoezi makali kwenye uwanja wa Uhuru leo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume waliounganisha Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na kuwa Tanzania huru , Sherehe hizo zitaadhimishwa Aprili 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru Mgeni rasmi akiwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)Katibu Mkuu Kiongozi wa Bw. Ombeni Sefue wa Tano kutoka kulia na Naibu Katibu Mkuu Kiongozi Dr. Frolence Turuka wa nne kutoka kulia na maafisa mbalimbali wa majeshi ya ulinzi na usalama wakijumuika pamoja kushuhudia mazoezi hayo ya vikosi vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa Uhuru.Mazoezi ya vikosi hivyo yakiendelea.Kikosi cha Askari wa msituni kikifanya mazoezi ya kutoa heshima kwa Amiri jeshi mkuu.Kikosi cha makomandoo kikitoa heshimaPicha mbalimbali zikionyesha vikosi vya zana mbalimbali za kivita vikifanya mazoezi ya kutoa heshima kwa mgeni rasmi Amiri Jeshi Mkuu.
Comments