Monday, April 14, 2014

Rais Jakaya Kikwete,Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa Walivyoshiriki Kumbukumbu ya Miaka 30 ya Kifo Cha Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine


Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili kushiriki misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishiriki misa maalum ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika nyumbani kwake Monduli. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenera Mkungara, na motto wa Marehemu sokoine Ndugu Joseph Sokoine.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowasa, wakishiriki Misa maalum ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.

Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameketi na wajane wa hayati Edward Moringe Sokoine pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa katika misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.

Mhe. Rais akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Lowasa nae akiweka shada.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim nae akiweka shada la maua.

No comments: