AJALI MBAYA MAKONGO, GARI DOGO LADONDOKEWA NA LORI LA MCHANGA, TAZAMA PICHA HIZI


 Hii ni ajali iliyotokea eneo la Makongo ambapo gari ndogo imeangukiwa na gari la mchanga asubuhi hii. Juhudi za uokoaji za askari we jeshi la wananchi wakisaidiana na kikosi cha zimamoto na uokoaji walifanikiwa kumtoa dereva wa gari dogo mida ya saa 1:20 za asubuhi baada ya kukaa humo tangu saa 11 asubuhi.
Gari liliangukiwa na kufukiwa na mchanga uliokuwemo kwenye gari lililopata ajali. Dereva wa gari dogo inasemekana kuwa alikuwa akiwapisha wavukao barabarani, ghafla lori lililouwa likija wa nyuma likakosa breki likapanda tuta na kuliangukia gari hilo dogo..

SOURCE: http://eddymoblaze.blogspot.com/

Comments