Wednesday, April 02, 2014

Rais Jakaya Kikwete Kwenye Ziarani Nchini Uingereza Pamoja na Mambo Mengine Uingereza asema Uingereza inajivunia Kuwa nchi inayoongoza katika Uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Duke of York ambaye pia ni  Balozi wa Biashara wa Serikali ya Uingereza  HRH Prince Andrew katika kasri ya Malkia ya Uingereza ya Buckingham Palace jijini London 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Jiji la London Mstahiki Alderman Fiona Woolf alipomtembelea ofisini kwake Mansion House jijini London 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Bw. Hague alipomtembelea ofisini kwake jijini London kwa mazungumzo 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wadau mbalimbali wa biashara na uchumi  wa Uingereza aliokutana nao katika ukumbi wa  Chatham House  jijini London.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyabishara wakubwa na wawekezaji wa Uingereza aliokutana nao katika mkutano wa biashara na uwekezaji katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola jijini London 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi mpango wa bima ya afya na maafa wa WESTADI wa mfuko wa Jamii wa NSSF jijini London, akiwa na Mkurugenzi wa NSSF Dkt RAmadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo Bw. Abubakar Rajabu (kushoto) . Mwenye miwani kati ni Bw. Aboubakar Faraji aliyekuwa mwongoza sherehe wa siku hiyo ambapo Dkt Kikwete alikutana na kuzungumza na Watanzania waishio Uingereza.Picha na IKULU

No comments: