Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo(kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta (kulia) ofisini kwake mjini Dar es salaam kuhusu maendeleo ya Bunge Maalum.
Katibu Mkuu wa Bakwata, Suleiman Lolila akisalimiana na Sitta alipowasili ofisi za Makao Makuu ya Bakwata jijini Dar es Salaam leo.
Shehe Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Simba akiwa ofisini kwake akimsubiri mgeni wake, Sitta kama anavyoonekana pichani.
Sitta akisalimiana na Shehe Simba baada ya kufika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa kazini Makao Makuu ya Bakwata kwenye ziara ya Sitta.
***********
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta leo amefanya ziara kwa viongozi wakuu wa kidini kwa lengo kuwaambia kile kinachoendelea ndani bunge hilo ambalo linaendelea na shughuli zake mjini Dodoma.
Akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika ofisi za Makao Makuu ya Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Sitta amesema amelazimika kufanya hivyo akiamini viongozi hao wana kundi kubwa la watu nyuma yao hivyo ni vyema wakawa wanasisitiza amani na umoja ndani ya taifa.
Mwenyekiti huyo alianzia makao makuu ya Kanisa Katoliki na kuonana na Mhadhamu Kadinali Pengo na kuzungumza naye faragha na baada ya hapo alimtembelea Shehe Mkuu wa Tanzania, Issa bin Simba na kufanya naye mazungumzo ya faragha pia.
Baada ya hapo, kiongozi huyo aliongea na waandishi wa habari na kusisitiza kuhusu kamati zilizoundwa kwa lengo la kufanikisha mchakato mzima wa kupata katiba mpya.
Comments