Mchoro wa namna litakavyokuwa jengo la Eco Residence litakaloanza kujengwa katika kitalu namba 67 kwenye makutano ya mitaa ya Ngano na Wakulima, Dar es Salaam litakapokamilika litakuwa na ghorofa 16, sehemu za makazi 118 na kuwa makazi ya watu zaidi ya 840 wakati kabla lilikuwa makazi ya familia moja.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), David Shambwe, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi mpya za shirika hilo zilizopo jijini Dar es Salaam leo, kuhusu uuzwaji wa nyumba za shirika hilo katika mradi wa Eco Residence zilizopo Kinondoni Hananasif Dar es Salaam.(kushoto) ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo Tuntufye Mwambusi na Kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa NHC, Muungano Saguya.
Ujenzi wa jengo hilo uliovpofikia kwa sasa
Timu ya mauzo ya Shirika la Nyumba la Taifa ikiwa katika eneo hilo
Mhandisi Anna Mrema wa kampuni ya ujenzi wa Estim Construction Ltd inayojenga jengo hilo la makazi akiwa anazungumza na vyombo vya habari asubuhi hii kuhusiana na ujenzi wa jengo hilo
Eneo la Ujenzi mtaa wa Ngano na Wakulima
Ujenzi wa jengo hilo uliovpofikia kwa sasa
Timu ya NHC pamoja na wakandarasi wa mradi huo wa wakulima
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UUZWAJI WA NYUMBA
ZA ECO RESIDENCES, DAR ES SALAAM
Kwa mara nyingine tena leo Jumanne ya
tarehe 1, Aprili, 2014, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linayo furaha ya
kuwatangazia rasmi Watanzania wote mauzo ya sehemu za nyumba za makazi (units) 118
za mradi ujulikanao kama Eco
Residence, uliopo katika eneo tulivu la Hananasif – Kinondoni, Dar es Salaam.
Nyumba
hizo za gharama ya kati na juu zipo Kilomita 6 kutoka katikati ya jiji
la Dar es salaam, zikiwa karibu kabisa na maeneo ya Oysterbay, Upanga na
Masaki.
Tungependa kuwajulisha watanzania kuwa
uzinduzi wa mauzo ya sehemu ya nyumba hizi hii leo unawapa tena fursa ya
kujiandaa kwa zaidi ya wiki tatu ambapo mauzo rasmi yataanza tarehe 23 Aprili, 2014.
Hivyo, tunawakaribisha watanzania wenye nia ya kununua nyumba za
mradi huo kuwa ifikapo tarehe hiyo waanze kulipia asilimia kumi kama malipo ya awali na baadaye
wamalizie malipo yao kupitia mikopo kutoka kwenye benki washirika 12 ambazo NHC imeingia makubaliano nazo. Kwa
kufanya hivyo watanzania hao wataweza kupata fursa ya kuwa wamiliki wa nyumba
hizo bora na za kisasa kabisa zinazojengwa na Shirika katika eneo lenye ardhi
yenye thamani kubwa.
Nyumba hizi tunazotangaza hii leo ziko za
aina na ukubwa mbalimbali zinazolenga
kukidhi mahitaji ya wananchi mbalimbali wenye uwezo wa kulipa kuanzia kiasi cha
shilingi millioni 199 mpaka million 253 bila VAT ili kuwawezesha
kila mwananchi kuwa na uchaguzi mpana kulingana na uwezo wake. Kwa wanunuzi wataonunua
nyumba ndani ya siku tisini watapata punguzo la asilimia 6.
Nyumba za Eco Residence zina
vyumba vitatu chumba kimoja kikiwa kimejitosheleza na kuna huduma zote muhimu. Tunawahamasisha
na kuwakaribisha watanzania wote walio nchini na walio nje ya nchi wafanye
mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika, Ofisi zetu za Mikoa au kupitia baruapepe
na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio
wazi wa manunuzi.
Ukiwa mdau na mnunuzi
mtarajiwa ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua nyumba katika mradi huu,
tafadhali waweza kuwasiliana na Kitengo
cha Mauzo simu namba
0754 444 333; baruapepe: sales@nhctz.com na pia tembelea
tovuti ya Shirika www.nhctz.com au Ofisi za NHC zilizoko mikoa yote Tanzania kwa
maelezo zaidi.
Mauzo ya Nyumba hizi yanafanywa na Shirika la Nyumba la
Taifa peke yake, hakuna dalali au wakala yeyote anayehusika au atakayehusika na
mauzo ya nyumba hizo.
BW. DAVID SHAMBWE
MKURUGENZI WA UENDELEZAJI BIASHARA
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
Comments