Tuesday, March 01, 2016

TANESCO YAOMBA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME KWA ASILIMIA 1.1.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Umeme Nchini (Tanesco) laomba kufanya mabadilko ya gharama za  umeme kwa kupunguza asilimia 1.1 kuanzia Aprili 1 mwaka huu kutokana kushuka kwa gharama za mafuta pamoja na Gesi ya Mtwara.

Tanesco imeiomba  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambao ndiyo lenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema kuwa wamepokea na kufanyia kazi kwa wadau kuweza kujadili maombi hayo ikiwa wameomba na mwakani kupunguza gharama za umeme kwa
 
 asilimia 7.9
 
.

Ngamlagosi amesema kuwa wanatarajia kukusanya maoni kwa wadau Machi 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam na baadae kuweza kuchambua juu kupunguza bei hiyo.

Amesema kuwa baada ya kuchambua kitaalam wataweza kubaini maombi hayo kupanda kwa asilimia hiyo kubaki kutokana na uendeshaji wa shirika hilo.

Ngamlagosi amewataka wadau kutuma maombi yao kwa maandishi katika ofisi yake katika tovuti ya EWURAwww.ewura.go.tz.

Aidha amesema kuwa gharama za mafuta kwa mwezi huu zimeshuka kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Lita moja ya Petrol ni sh.1,881, Dizeli sh.1,486 pamoja na Mafuta ya Taa sh.1,465.


Amesema bei za mafuta zinatofautiana kutokana na umbali wa Mkoa na Wilaya hivyo katika kujua bei hiyo wataweza kujua kupitia namba *152*00# na wateja wametakiwa kudai stakabadhi za malipo katika kuhakikisha serikali inapata mapato hayo.
Post a Comment