Thursday, September 03, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO YA WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUDUMU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) NA WATAALAMU WA HAKI NA SHERIA, JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) wakati alipokuwa akiwasili kwenye Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli hiyo uliokuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi. Wa tatu (kulia) ni Jaji Mkuu Mstaafu  Agustino Ramadhan. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi. 

No comments: