Friday, September 04, 2015

LOWASSA, MBOWE WAANZA KUPASUA ANGA KWA CHOPA, MPANDA "KWAFURIKA" , WAELEKEA KIGOMA

Kwa mara ya kwanza tangu mgombea wa kiti cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CHADEMA, akiwakilisha vyama vya UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akifuatana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wameanza kuruka kwa chopa "kushambulia' mikoa ya Magharibi ambapo jana Septemba 3, 2015, wametua Mpanda, mkoani Katavi na kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye shule ya msingi Shule ya Msingi Kashaulili

CHOPA, ilioyowachukua Mh. Lowassa, na Mwenyekiti Mbowe, ikiruka baada ya kuhutubia mkutano wa kampeniMmoja wa wananchi akibebwa baada ya kuzirai kutokana na msongamano katika mkutano wa kampeni za mgombea urais, Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda mkoani Katavi

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mgombea wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Mtapenda, Bi. Pauline Pesnacy, mara baada ya kumnadi kwa wananchi wa Mpanda, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi jana Septemba 3, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni na kunadi sera zake.(Picha zote na Othman Michuizi na Fidelis Felix)
Post a Comment