Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza-kuu) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata mikoa mingine. Pia Waziri Chikawe katika mkutano huo, alitangaza kupiga marufuku wapiga ramli wote nchini kwa kuwa wanasababisha kuendelea kwa matukio ya kinyama wanayotendewa albino. Hata hivyo, katika mapambano ya kusambaratisha unyanyasaji huo, waziri huyo alitangaza kushirikiana ipasavyo na viongozi wa dini pamoja na mashirika ya kijamii ili kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kutokana na uhalifu huo dhidi ya albino. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Tuesday, January 13, 2015
SERIKALI YAUNDA TIMU KUTEMBELEA MAENEO SUGU YA UTEKAJI, UUAJI ALBINO, YAPIGA MARUFUKU WAPIGA RAMLI NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma
Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya mazungumzo na Fitch Ratings Ltd amb...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...
No comments:
Post a Comment