




Meneja masoko na utafiti wa shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elisante Maleko amewataka watanzania kuona shirika hilo ni mali yao kwa kuwa shirika hilo ni mali ya umma na michango ni midogo hivyo kila mwananchi kumudu
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliyotembelea banda lao katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid jijini Arusha
Bw.Maleko alisema kuwa shirika hilo lina bima ya matibabu amabayo ni mpango maalum wa shirika hilo kutoa kinga ya matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kuumwa na michango ni midogo na kila mwananchi anamudu kujiunga na huduma zinapatikana nchi nzima
Pia alisema Bima za nyumba inakinga na majanga ya wizi,moto,tetemeko na mafuriko hivyo kuwataka wananchi kukatia nyumba zao bima.
No comments:
Post a Comment