Tuesday, September 23, 2014

KINANA AITEKA CHALINZE PWANI, LEO KUENDELEA MKOANI TANGA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kiwangwa ambapo alikagua jengo jipya la wodi ya Wazazi. Kituo cha afya cha Kiwangwa kina uwezo wa kuhudumia watu zaidi ya elfu kumi.
 Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Kiwangwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akishiriki ujenzi wa jengo la kituo cha afya kata ya Miono.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa kata ya Miono
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Miono ambapo aliwaambia wawe makini katika kuchagua viongozi wa kijiji ili kuepusha migongano na migogoro ya ardhi zinazodaiwa kuuzwa kwa wawekezaji
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka Miono baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi wa hapo.
 Soko la Mbwewe ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilikagua, soko hili limegharimu zaidi ya shilingi milioni 200.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi Msata ambapo alisisitiza wazazi kuwasomesha watoto wao .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye eneo la shule ya msingi Msata mara baada ya kukagua madarasa mawili na maktaba ya kujisomea.
 Kada maarufu wa CCM na Msanii wa ushairi Latifa Kizota akighani utenzi unaofahamika kama Kidumu chama chetu wakati mkutano uliofanyika Chalinze mjini.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akiwasabahi wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara mjini Chalinze.
 Umati wa wakazi wa Chalinze ukimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Chalinze.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi wa Chalinze.
 Wakazi wa Jimbo la Chalinze wakisikiliza kwa makini
 Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wakazi hao na kuwasisitiza juu ya masula muhimu ikiwa kuchagua viongozi bora, kuwapeleka watoto shule ,kujiandikisha huduma za afya ya jamii na matumizi bora ya ardhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa Makatibu Kata.

No comments: