Tuesday, September 23, 2014

MRADI WA NYUMBA WA DEGE ECO- VILLAGE WAANZA, WANANCHI WACHANGAMKIA FURSA.

Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyofanyika jijini Dar es Salaam inategemea kuanza hivi karibuni.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. 
Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.
Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wa kazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village wakiwahudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village akibadilishana mawazo na mfanyakazi mwenzake.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akiongea na mteja ambaye alikuwa akiweka kumbukumbu katika daftari la wageni waliofika banda la Dege Eco – Village ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Dege Eco-Village wakiwa katika picha ya pamoja.
Wananchi wakionyeshwa mpangilio wa nyumba utakavyokuwa.
Muonekano wa banda la Dege Eco-Village.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco -Village Bw. Adam akiongea na waandishi wa habari kufafanua jambo. 
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akibadilishana mawazo na wateja waliofika katika banda lao.

No comments: