Saturday, September 27, 2014

EVELYN BAASA NDIYE REDD’S MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2014

 
Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya
Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi
wa taji hilo, Evelyn Baasa (katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole
Sarakikya, Lilian Kamazima, Lilian Timothy na Dorice Mollel.
 Warembo wakilisakata rumba kabla ya kuatangzwa kwa matokeo hayo.
 Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania Photogenic 2014
Father Kidevu Blog, Arusha
Mlimbwende
Evelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na
kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2014.
Kwa
kushinda taji hilo Baasa ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika
Kitongoji cha Karatu naabadae kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa
mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014.
Shindano
hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo
washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo
fanyika mapema mwezi ujao.
Miongoni
mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss
Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.
Kwa mujibu
wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la Miss
Tanzania, Hashim Lundenga ‘Uncle’ amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga
picha na wadau wa masuala ya urembo  wa
masuala ya urembo Tanzania walikaa na kumchagua mshindi huyo kupitia picha
mbalimbali za warembo hao.
Majaji
waliowezesha kupatikana kwa mshindi huyo ni Mpigapicha mkongwe wa masuala ya
urembo nchini Mroki Mroki ambaye anafanyakazi na Magazeti ya Serikali ya Daily
News na Habarileo, Mtayarishaji wa vipindi Elliud Pemba wa True Vision na Afisa
Itifaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mukhsin Kassim.
Taji la
Redd’s Miss Tanzania Photogenic lilikuwa linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania
2013 Happyness Watimanywa.
Warembo wengine
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Miss Photogenic ni Dorice Mollel, Nicole
Sarakikya, Lilian Timothy na Lilian Kamazima.
Kesho warembo hao watachuana tena kuwania taji la Miss Top Model katika shindano
litakalofanyika Triple A jijini Arusha.

No comments: