Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Juma Seleman Nkamia(katikati) na Mjumbe Mwenzie SaidAmour Arfi(kulia) wakibadilishana mawazo jana mjini Dodoma na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Shaban Kissu (kushoto) mara baada ya kikao cha 41 ambacho kimepitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge ili ziwawezeshe wajumbe walioko nje kupiga kura ya kupitisha vifungu mbalimbali vya Katiba inayopendekezwa.Picha na MAELEZO-DodomaWaziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt.Fenella Mukangara (kushoto) akibadilisha mawazo na Mjumbe mwenzie Paul Makonda(katikati) na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff), Simon Mwakifwamba (kulia) mara baada ya kikao cha 41 ambacho kimepitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge ili ziwawezeshe wajumbe walioko nje kupiga kura ya kupitisha vifungu mbalimbali vya Katiba inayopendekezwa.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba John Cheyo (kushoto) na Paul Kimiti (kulia) wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi mara baada ya kikao cha 41 ambacho kimepitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge ili ziwawezeshe wajumbe walioko nje kupiga kura ya kupitisha vifungu mbalimbali vya Katiba inayopendekezwa.
Comments