Thursday, September 18, 2014

MSTAHIKI MEYA WA ILALA JERRY SILAA ASHUSHA NEEMA KWA SHULE YA MSINGI KIVULE‏‎

 Kwenye picha ni baadhi ya madawati yaliyotolewa na Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa katika shule ya kivule iliyopo manispaa ya Ilaa jijini Dar es Salaam
 baadhi ya wanafunzi wakiwa wanaendelea kusikiliza tukio liendavyo
 Kikundi cha ngoma cha makirikiri kilichoundwa na wanafunzi kwaajiri ya kusherehesha katika sherehe hiyo ua kukabidhi madawati mkatika shule ya kivule
 Burudani ikiwa imepamba moto
 
 kundi la burudani ka kikulwa likiwa linatoa burudani wakati wa kukabidhi madawati hayo
 Mh:Jerry Silaa akiwa ameongozana wa viongozi mbalimbali walio kuwepo katika shughuli hiyo kwenda kukagua madarasa mawili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni 
 Akizungumza na viongozi hao mara baada ya kuangalia madarasa hayo ambayo nayo ameshirika katika kuchangia wakati wa ujenzi
haya ndiyo madarasa ya vyumba viwili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni katika  shule ya kivule
Akikabidhi madawati hayo MH:Jerry Silaa amewaasa kuwa
hata yeye alikuwa anasoma na anakaa chini lakini kwa kizazi cha sasa yatupasa
tubadilike hiyo hatapenda kuona watoto wakiendelea kukaa chini  na kusoma katika mazingira magumu kama aliyo
weza kusoma yeye  kwahiyo kwa moyo wake
anarudisha fadhira kwa watanzania  kwa
kushirikiana na wadau mbal;imbali kwa misaada tofautitofauti katika kipindi
chake cha uongozi kwa nafasi ya meya
Aidha muheshimiwa aliweza kuwafafanulia baadhi ya watu walio
weza kufika katika hafra ya kukabidhi madawati kwa shule ya kivule kwamba kodi
za pango zinavyo kusanywa huwa haziliwi na mtu zaidi ya kutatua matatizo katika
sehemu mbalimbali ya halmashauri kwahiyo aliwaomba watu wote wasiwe na imani ya
kuliwa kwa fedha hizo bali watambue zinakazi nyingi na tofauti tofauti katika
halmashauri husika
Naye mwalimu mkuu wa shule ya kivule wakati akisoma risala
waliyo iandaa kwaajiri ya shughuli hiyo alisema shule ya kivule inawanafunzi
wengi ambao ni takribani ya wanafunzi 2020 ambapo inakabiriwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa madawati ,matundu ya vyoo,nyumba za walimu
ambapo kwa sasa kuna nyumba moja tu,waalimu wa masomo mbalimbali pamoja na
vifaa vya kufundishia hususani  somo la
Tehama,hivyo kupelekea waalimu kutumia nguvu katika ufundishaji
Bw.kubilu Lupembe  Dede
ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya kivule ametoa shukrani za dhati kwa
mstahiki meya  wa ilala Jerry Silaa
ambapo ameonesha nia ya dhati katika kufanikisha elimu inasonga mbele kwa
kujitoa sehemu mbalimbali  na kuwa karibu
na jamii

Pia diwani wa kata ya kivule Bw.Nyansika.G.Motena ametoa
shukrani kwa niaba ya wananchi wote kwa kile anacho kifanya mheshimiwa meya wa
ilala Jerry Silaa ameweza kukifany ana kusema inapaswa kuwa kiongozi wa mfano kwa wengine  

No comments: