Friday, September 26, 2014

MSANII WA MAREKANI T.I KUTUMBUIZA LIVE DAR ES SALAAM KATIKA FAINALI ZA FIESTA.

DSC_1486
Mkurugenzi Mkuu wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Efraim Mafuru (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Ruge Mutahaba katika hoteli ya Serena wakati wa kumtambulisha msanii TI wa Marekani ambaye atashiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
DSC_1484
Mkurugenzi Mkuu wa Masoko ya Kampuni ya Serengeti (SBL), Ifraim Mafuru (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Prime Time Ruge Mutahaba ( wa tatu kushoto), meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo (wa pili kutoka kushoto), Elihuruma Ngowi (kushoto) na kulia ni meneja masoko wa Serengeti Allan Chonjo, wakati wakitangaza ujio wa mwanamuziki wa Marekani TI akayeshiriki katika tamasha la Fiesta litakalofanyika Oktoba 18  jijini Dar es Salaam.
DSC_1480
Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Allan Chonjo akizungunza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakimtangaza mwanamuziki TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
DSC_1476
Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Ifraim Mafuru (kushoto) akisalimia na Mkurugenzi wa Prime Time Ruge Mutahaba wakati wa kumtangaza mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
DSC_1472
Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Ifraim Mafuru (katikati) pamoja na Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rogamba (kushoto) na meneja masoko Allan Chonjo wakati wa kumtambulisha mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
DSC_1461
Mkurugenzi wa Prime Time na meneja wa vipindi wa Radio Clouds FM Ruge Mutahaba akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika Dar es Salaam mwezi ujao.
DSC_1453
Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Allan Chonjo (kulia), Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Ruge Mutahaba (katikati) na meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rogamba wakati wa hafla ya kumtangaza msanii wa Marekani TI kutumbuiza katika tamasha la Fiesta mwezi ujao Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
DSC_1448
DSC_1441Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ifraim Mafuru akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafala ya kumtangaza msanii wa Marekani TI ambaye atashiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
 TI, KUTUMBUIZA FAINALI ZA FIESTA 2014
Mwanamuziki wa Kimarekani katika miondoka ya Hip-hop ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, mwigizaji na mwekezaji, Clifford Joseph Harris Jr, alimaarufu kama T.I. amethibitishwa rasmi na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd (SBL)kama mwanamuziki wa kimataifa atakayetumbuiza katika kilele cha shangwe za Serengeti Fiesta zitakazofanyika jijini Dar es salaam tarehe 18 Oktoba mwaka huu.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya SBL, Meneja Masoko Allan Chonjo alisema, ” hivi karibuni tumetia saini na kukamilisha mikataba yote ili kuhakikisha kwamba mwanamuziki huyu wa kimarekani anafika Leaders Club jijini Dar essalaam tarehe husika”
Chonjo aliendelea kusema, ‘Tungependa kuwashukuru washirika wetu, Prime Time Promotions kwa kuhakikisha tunakamilisha mikataba yote na vile vile kwa kuhakikisha kamba tamaha hili linakamilika kwa mafanikio. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwamba T.I kutia mguu wake katika ardhi ya Tanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari, Sebastian Maganga kutoka Prime Time Promotions, alikuwa na haya ya kusema, “kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa tukihakikisha kwamba tunaelewa nini watanzania wanataka na tumekuwa tukijitahidi bila kuchoka kuhakikisha kamba tukio tunalolifanya, kwa mwaka huu, wapenzi wetu watashuhudia shoo ya nguvu ambayo haijawahi yanyika hapa nchini.
“mpaka sasa, Serengeti imetembelea mikoa kumi (10) nchini, na itaendelea na ziara hiyo katika mikoa ya Singida, Songea, Mtwara, Dodoma na Mbeya.
Katika mabadiliko mengine Serengeti Breweries na Prime Time Promotions wamewaomba mashabikiwachague msanii wa kitanzania ambaye wangependa atumbuize na TI. “Hiki ni kitu kipya natunataka kuhakikisha kwamba mashabiki wanaburudika vya kutosha, alisema Maganga. ‘Habari zitasambazwa kwa njia ya TV na redio kuelezea jinsi ya kushiriki’, aliongeza.
  Serengeti Fiesta inatambulika kwa kuleta wasanii wa kimataifa hapa nchini, miongoni mwao ni pamoja na Rick Ross, Shaggy na Davido
T.I aliyetamba na kibao “No Mediocre” amekuwa akijishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo biashara. Yeye ni muasisi na mkurugenzi mkuu wa Grand Hustle Records.
T.I. alianza kupata umaarufu mwaka 2003, baada ya kushirikishwa na mwanamuziki mwenzake Bone Crusher, ambaye ni mkazi wa Atlanta, katika wimbo wa “Never Scared”. Alipata umaarufu zaidi baada ya kutoa wimbo wa Trap Muzik (2003).
Mwaka 2004, T.I. alionekana kwenye wimbo wa Destiny’s Child’s “Soldier”, sambamba na Lil Wayne. Albamu ya sita ya TI, Paper Trail (2008), ilikuwa albamu yake ya mafanikio zaidi , na imefanikiwa kuuza nakala 568,000 katika wiki ya kwanza nchini Marekani na kuifanya ya tatu katika chati ya albam bora nchini humo. Mpaka sasa, T.I. amdeshinda tuzo tatu za Grammy Awards.
 T.I. pia ametoa nyimbo kama vile”Bring Em Out”, “What You Know”, “Swagga Like Us” (akimshirikisha Kanye West, Jay-Z and Lil Wayne), “Dead and Gone” (akimshirikisha Justin Timberlake), “Ball” (akimshirikisha Lil Wayne) and “No Mediocre” (akimshirikisha Iggy Azalea).
KUHUSU SERENGETI BREWERIES LIMITED 
Serengeti Breweries Limited ni kampuni ya bia ambayo huandaa, kuzalisha na kuuza vinywaji vilivyotenezwa na shairi, ngano na mtamaa nchini Tanzania.
Kikiwa na makao yake makuu jijini Dar es Salaam, SBL hutengeneza vinywaji vifuatavyo:- Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick and Guinness®.
 SBL pia husambaza vinywaji mbalimbali vikali za kimataifa kama Smirnoff Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and Gilbeys Gin®.
Serengeti Breweries Limited ni kampuni mwenza ya East African Breweries Limited/ DIAGEO PLC.

No comments: