MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUTEMBELEA HIFADHI YA KATAVI

WATALI_WA_NDANI[1]Madiwani wa wa Halmashauri ya Mpanda wakiwa katika Picha ya Pamoja nje ya ofisi ya hifadhi ya wanyama pori Katavi kabla ya kuanza safari ya kutembelea hifadhi hiyo.MAMBA
VIBOKO_HOI[1]Hapo wanyama aina ya viboko wakionekana kuhangaika kutokana na ukosefu wa maji ya kutosha kwenye Mto Ikuu na kavuu ambayo inaitwa Shule ya Viboko na Mamba,SIMBA_KATAVI[1]Huyo ni mnyama mfalme wa pori simaba akiwa amejipumzisha kivulini huku akiwa katika  mawindo  yake kama ilivyo kawaida yake.VIBOKO[1]Hao ni viboko wakilandalanda nje yam to Ikuu ambao umekauka maji na wengine wakiwa majini kama wanavyoonekana hapoTEMBOOOMnyama aina ya Tembo wakiwa kwa mbali wakikimbia kutafuta maji ili kuweza kupoza koo zao baada kupata lishe na kwa nyuma watoto wa Tembo wakifuata.
Madiwani wa Halamshauri ya Wilaya ya Mpanda watembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kujionea wenyewe athari  ya uharibifu wa mazingira unavyoathiri wanyama katika mbuga ya katavi hasa wanyama aina ya Viboko na mamba kutoka na ukame unaikabiri mbuga hiyo kupelekea wanyama hao kwenye mto Ikuu Katavi na ziwa Chanda kukauka na kuwafanya wanyama hao kufa kutokana na ukosefu wa maji.
Madiwani wapatao 13 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri wakifuatana na watalaam kutoka Idara ya Maliasili na Mazingira,Kilimo, na Idara ya Utumishi na Utawala walifanya safari kutembelea mbuga hiyo na kujionea hali ilivyo katika hifadhi hiyo ambapo walifika eneo linaloitwa mto ikuu unaopokea maji kutoka mto Katuma ambao ndi tegemeo kuu la kupeleka maji kwenye mbuga hiyo ukiwa umekauka kutokana na uharibifu mkubwa unaofanywa na wananchi kwenye vyanzo vya mto huo.
Maeneo yaliyoathiriwa sana na ukame ni eneo la  Mto Ikuu ,Kuu,na Chanda ambapo makundi ya wanayam aina ya viboko walikuwa na hali mbaya wakihangaika kutafuta maji huku wengine wakiwawamelala hoi bin taabani .
Mbali ya wanyama aina ya Viboko ambao ni wengi katika mbuga hiyo pia wanyama  Mamba ,makundi ya Tembo,Nyati,Twiga, Pundamilia,na wengineo pamoja na makundi ya ndege walikuwa wamekusanyika kwa pamoja huku yakipigania maji kidogo yaliyosalia katika vidimbwi vya mto huo angalau waweze kutuliza kitu waliyokuwanayo dhahiri shahiri wanyama katika hifadhi ya Katavi wanahali mbaya.
Hifadhi hiyo ambayo ni kubwa nay a tatu kwa ukubwa hapa nchini ni rasilimali pekee na hazina kubwa kwa taifa kutokana na wanyama waliomo,wakubwa wakubwa kama nyati, tembo Simba ,kongoni viboko ,makundi ya ndege na mimea ya aina mbali mali amabyo ni kivutio kikubwa kwa watalii lakini inakabiliwa na uharibifu mkubwa kutokana na kukoasa maji kwa wanyama hao kwa kile kilichoelezwa uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kwenye vyanzo vya maji vya mto katuma ambao unapeleka maji kwenye mbuga hiyo.
Akizungumzia hali ya uharibifu unaofanyika wa mazingira katika hifadhi ya Katavi Mhifadhi wa ujirani mwema katika hifadhi ya Taifa ya Katavi David Kadomo ameelaz kuwa Hifadhi ya Taifa ya Katavi inakabiliwa na changamoto ya ujangili mkubwa hasa wa kuuwawa kwa Tembo,na upo wasiwasi mkubwa kuwa huenda Tembo hao wakatoweka kutokana na ujagili unaofanyika katika hifadhi hjiyo.
Mbali ya ujagili pia hifadhi inakabiliwa na changamoto ya wafugaji kuingiza mifugo ya kwenye hifadhi hiyo ya Taifa ya Katavi na kufanya mahali pa malisho, wapo wafugaji wengi wanavamia hifadhi na makundi yao ya ngombe katika hifadhi hiyo pamoja na juhudi zinazofanyika kuilinda bado watu wanaingia na mifugo yao.
Mhifadhi Kadomo akaeleza kuwa pia maeneo yaliyohifadhiwa ambayo hayako kwenye hifadhi amabayo ni maeneo ya uhifadhi wa wanyapori ambayo yako mita miatano kutoka eneo la hifadhi na kijiji ya WMA ya Ubende na Mpimbwe yanaonekana kuvamiwa na kufanywa shughuli za kibinadamu za kilimo,mifugo na makazi ya watu jambo ambalo siyo taratibu kwa kuwa hayaruhusiwi kufanywa kwa shghuli hizo za kibinadamuzinazoathiri mazingira.
Kwa kuwa sheria ya uhifadhi wa wanyama pori imeeleza wazi kuwa mita 500 zilizotengwa kutoka  nje ya  hifadhi shughuli zinazofanyika hapo zisiwe zile zinazoweza kuathiri mazingira lakini maeneo mengi kwenye hifadhi hizo za wanyama yanaharibiwa na viongozi wanaona wapo.
Wananchi wanagawiwa mashamba katika maeneo hayo na viongozi wanaangali akaawaomba madiwani kwa kuwa wako karibu na wananchi wawaelimisha juu ya kutoharibu mazingira na umhimu wa uhifadhi ili wasiendelee kuharibu mazingira katika hifadhi hizo na ile ya Katavi.
Pia alielezea changamoto ya uchomaji moto mapori na hata maeneo yaliyojirani na hifadhi ,vilevile utupaji taka hovyo ndani ya hifadhi pamoja na mwendo kasi wa magari yanayopita katika hifadhi hiyo kwa kuwa hifadhi inapitiwa na barabara mbili ziendazo sumbawanga na ile ya Tabora wanyama wanagongwa sana akashauri madereva wanaotumia mbarabara hizo wajitahidi kuzingatia sheria na kupunguza mwendo waende mwendo wa kawaida ili kuepuka kuwagonga wanyama katika hifadhi hiyo.
Kwa UPANDE WAKE Diwani wa Kata ya Kabungu Selemani Kasonso alieleza kuwa watajitahidi kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha wanaokoa maisha ya wanyama hao ambao wanategemea maji yam to katuma na kwenye kata yake wapo watu wanaoharibu mazingira yam to huo kwa kuweka vikingamaji ili maji yasiweze kupita kwa ajili ya kilimo cha mpunga akasema watalipigia kelele kwelikweli kwenye vikao vyao mpaka wafanikishe,.
Akaongeza kuwa wanyama hao wanateseka sana na wanakufa haiwezekani rasilimali kama hii ipotee hivi kizazi kijacho kitakuja kutuhumu kwa kushindwa kutunza wanyama hao na kuhifadhi mazingira ili waendelee kuwepo milele na milele,akasema mfano wazungu waliwauwa wanyama wote kule kwao na kuharibu mazingira hatimaye wakatoweka sasa ndiyo maana unao wanakimbili huku kwetu hasa Tanzani kuja kuaangalia kwa kuwa hkule kwao hawapo tena,ni wajibu wetu sasa kuhakikisha tunalisimamia hili.alisema Kasonso.

Comments