Thursday, September 25, 2014

BUNGE MAALUM LA KATIBA LAPENDEKEZA IBARA 274 BADALA YA 271 ZA TUME

jBUNGE MAALUM LA KATIBA LAPENDEKEZA IBARA 274 BADALA YA 271 ZA TUME .
  • IBARA 186 ZA TUME ZABORESHWA
  • IBARA 41 MPYA
  • IBARA 47 ZA TUME ZABAKI KAMA ZILIVYO
  • IBARA 28 ZA TUME ZAFUTWA
Na Mwandishi wa MAELEZO-Dodoma
Bunge Maalum la Katiba limependekeza jumla ya Ibara 274 katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum Mhe. Andrew John Chenge wakati akiwasilisha Bungeni Rasimu ya Katiba inayopendekezwa katika Kikao cha Arobaini na mbili.
Amesema kuwa wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawasilisha Bungeni Rasimu Katiba inayopendekezwa iliwasilisha Ibara 271.
Mhe. Chenge amesema kuwa baada ya kupitia Rasimu Katiba ya Tume walifanikiwa kupata Ibara 274 ambazo ndio wanapendekeza ziwemo katika Katiba mpya ijayo.
Ameongeza kuwa kati ya hizo zilizopendekeza na Bunge Maalum la Katiba 233 zimetokana na mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyowasilisha Bungeni mwezi Machi mwaka huu.
Amesema kuwa katika Ibara 47 kati ya zote za Tume 47 hazikufanyiwa marekebisho badala yake zilibaki kama zilivyopendeza wakati Ibara 186 ndio zilifanyiwa maboresha na marekebisho kwa ajili ya kuziboresha na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Mhe. Chenge ameongeza Bunge hilo limeongeza Ibara 41 mpya na kufuta 28 zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 Rasimu ya Katiba inayopendekeza na Bunge Maalum la Katiba ina sura mpya mbili mpya ambayo ni ardhi ,maliasili na mazingira na sura inayohusu Serikali ya Mapinduzi ya Mapinduzi, Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawakilishi.

No comments: