KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KOROGWE, KUENDELEA WILAYANI LUSHOTO

3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mama  Veronica Simba wa Majengo Mombo wilayani Korogwe wakati alipomtembelea jimbo la Korogwe vijijini linaloongozwa na Mh. Steven Ngonyani Maarufu kama Prof. Maji Marefu, katika mradi wake wa kufundisha wanafunzi wa ushonaji wa nguo akiwa katika ziara yake mkoani Tanga akikagua utekelezaji wa  ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuhimiza huai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MOMBO-KOROGWE)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo wakati alipomtembemea mama Veronica Simba katika eneo la majengo mjini Mombo leo huku wanafunzi wa mama Veronica Simba wakifurahia tukio hilo.1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo wakati alipomtembemea mama Veronica Simba katika eneo la majengo mjini Mombo huku mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Mh. Steven Ngonyani akifurahia.
14Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi katika  wa maabara katika shule ya sekondari ya Chekereni mjini wilayani Korogwe.13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu kulia na Mrisho Gambo Mkuu wa wilaya ya Korogwe wakati alipowasili katika shule ya sekondari ya Cherereni Mombo.12Waandishi wa habari waliokatika msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Said Mwishehe wa Jambo Leokulia na David John wa Majira wakizungumza na wanafunzi katika shule ya sekondari Machewa.11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani alipokuwa akitoa maelezo kuhusu sekondari ya Mashewa wilayani Korogwe, Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Ndugu Mrosho Gambo.9Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akimimina zege wakati akishiriki katika ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Mashewa huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuhudia tukio hilo.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya w atendaji wa serikali wakati alipowasili katika shule ya sekondari ya Chekereni kukagua mradi wa ujenzi wa maabara ya shule hiyo.29Mmoja wa wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Mombo leo Bw.Mageda Hamza  akiuliza swali katika mkutano huo.28Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu katikati ni Mnec wa wilaya ya Korogwe vijijini Ndugu Edmund Mndolwa26Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akivishwa mgolole kama ishara ya heshima ya wasambaa kumkaribisha mgeni shujaa kwao wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.25Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo.24Wananchi waliohudhuria katika kutano huo wakinyoosha mikono yao juu kama salamu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana23Mmoja wa masjhabiki wa CCM akionyesha alama ya vidole viwili juu kama ishara ya kukubali jambo katika mkutano huo.18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakipungia wananchi mikono wakati alipowasili katika eneo la mkutano wa hadhara  mjini Mombo 22Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa akizungumza na wana Mombo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mombo jana.21Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akizungumza na wapiga kura wake mjini Mombo Korogwe jana.20Wananchi wakinyanyua mikono yao juu wakati wa mkutano huo.19Baadhi ya wasichana wa kimasai wakiwa katika mkutano huo. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mombo jana.

Comments