Friday, September 26, 2014

MASHEIKH NA MAPADRE KUSAKATA KABUMBU UWANJA WA TAIFA OCTOBA, 12 2014

DSC_0010Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Alhadi Mussa Salum (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya Masheikh na Mapadre utakaofanyika uwanja wa Taifa Octoba 12-2014. Alhadi Salum ndiye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi wa mchezo huo. Kushoto ni Katibu wa Kamati  ya Amani kutoka Kanisa la Anglikana Padri John Solomon na   Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania Stefan Reith.DSC_0011Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania Stefan Reith (kushoto), akimkabidhi baadhi ya vifaa vya michezo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamSheikhAlhadi Mussa Salim kwa ajili ya  maandalizi wa mechi hiyo.
OKTOBA 12 mwaka huu katika kuadhimisha siku ya amani duniani viongozi wa dini wanatarajia kujitupa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakiwa na lengo la kudumisha amani iliyopo nchini.
Mtanange huo utawajumisha Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wachungaji na Mapadre na mgeni rasmi katika mchezo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye tayari amekubali kuungana na viongozi hao wa dini.
Akizungumza jana jijini, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mchezo huo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said Sadick atakuwa mwamuzi msaidizi akisaidiwa na Kamishna wa Kanda Maalumu, Seleman Kova na Afande IGP Ernest Mangu atakuwa mpuliza kipyenga wa kati.
Alifafanua kuwa viongozi hao wa dini tayari wameshaanza mazoezi kwa jili ya kujiweka tayari kwa ajili ya kufanya vizuri katika mtangane huo wa kuhamasisha amani na ulivu nchini katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa wanaendelea na mazoezi hayo chini ya kocha mjerumani na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, itazipeleka timu mbili mkoani Morogoro kwa ajili ya kujifua zaidi na mtanage huo utakaokuwa wa kukata na shoka kutokana na jinsi timu za viongozi hao wa dini zilivyojipanga kucheza mchezo huo wa amani.
Ili kujindaa vema na mchezo huo Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania, Stefan Reith, jana alikabidhi Sheikh kwa Dar es Salaam, Alhad Salum vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jeszi na viatu.

No comments: