Thursday, September 18, 2014

ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KISIWANI MAFIA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria ishara ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya CCM wilaya ya Mafia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mafia.
 Hii ndio ofisi mpya ya CCM wilaya ya Mafia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akifanya mzaha na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada kukagua mradi wa maji,masaidia zaidi ya mradi huu wa maji  utahudumia watu zaidi ya 3000.
 Sehemu ya vifaa vya mkandarasi vikiwa kwenye eneo linapotengenezwa tuta la Banjo,ujenzi wa tuta hili utasaidia sana wakazi wa vijiji vya Banja na Jojo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya mashua kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya wa pwani
 Mafia umeme kila kona mpaka kwenye nyumba ya Udongo
Ufukwe wa  Mafia
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaaga wananchi wa Mafia tayari kwa safari ya kurudi Nyamisaki.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimwonyesha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman taarifa mbali mbali kutoka kwenye blogs, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na upande wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwinshehe Mlao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akiteremka kutoka kwenye mashua ambayo imewasafirisha salama kwa muda wa masaa manne.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiteremka kwenye mashua
 Katibu Mkuu wa CCM, akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari kutoka Kisiwa cha Mafia kwenda Nyamisati wilayani Rufiji, baada ya kumaliza ziara yake katika wilaya ya Kisiwa hicho, jana Septemba 17, 2014, akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoahuo. Boti hiyo ambayo pia hutumiwa na wananchi kusafiria kati ya kisiwa hicho cha Mafia na Nyamisati Kinana amesafiri nayo kwa saa nne tangu saa sita mchana hadi saa 11 jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM akipanda boti hiyo kwa ukakamavu
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye boti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, ambaye aliwasili wilayani Mafia kwa ndege lakini akalazimika kusafiri na Kinana kwa boti hiyo kurejea Nyamisati. Watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao.
 Katibu wa NEC, Itikadina Uenezi, Nape Nnauye (watatu kushoto), akiwa kwenye boti na abiria wengine waliosafiri pamoja na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati.
 Baadhi ya maofisa wa CCM na Waandishi wa habari wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa Makao Makuu ya CCM, Daniel Chongolo (watatu kushoto) akiwa na abiria wenzake katika boti hiyo kutoka Mafia hadi Nyamisati.
 Abiria wengine wakiwa katika boti hiyo kutoka Mafia kwenda Nyamisati. Kushoto ni Mwandishi wa Clouds TV/Radio Salum Mwinyimkuu.
 Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
  Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mama Salma Kikwete ya Wama iliyopo wilayani Rufiji, baada ya kutoka Mafia. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Suma Mesa. Kinana amempongeza Mama Salma kwa uamuzi wake wa kuanzisha shule hiyo ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto yatima kutoka mikoa mbalimbali nchini.
 Watoto wa shule hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu Kinana.
Kinana akiondoka kwenye shule hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao na watatu kushoto ni Mwandishi wa habari wa gazeti la Jamboleo, Saidi Mwinshehe na kulia ni Chongolo. Kinana anatarajiwa kuendelea na ziara yake katika mkoa wa Pwani leo, Septemba 18, 2014. Maelezo/Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog

No comments: