Monday, September 29, 2014

Msama awapiga jeki KKKT Segerea


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam na kuahidi kutoa sh. milioni 6 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala. 
 Mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASAT) Alex Msama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
 Mchungaji Emmanuel Masanja 'Masanja Mkandamizaji' aliguswa na kutoa ahadi ya shilingi milioni 1 katika hafla hiyo.
"Mimi na familia yangu tutatoa milioni 1".
 Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi, Mchungaji Christosiler Kalata akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sehemu ya mchango walioahidi katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Usharika huo ulitoa ahadi ya sh. laki 7.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akipokea mchango wa Usharikia wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Christosiler Kalata .
 Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.
 Watu mbalimbali waliahidi kutoa michango yao kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Kanisa hilo.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Edson Mwasabwite alichangia kiasi cha sh. laki moja.

Na Mwandishi Wetu  

  

MJUMBE wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Alex Msama ametoa kitita cha sh. mil 6 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika Segerea.



Msama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alitoa kiasi hicho katika harambee hiyo ya kufanikisha ujenzi huo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam, huku akitoa na ushuhuda wa maisha yake mpaka kufikia hatua aliyofikia sasa.



Akizungumzia ushuhuda huo, Msama aliwataka waumini kuiga mfano wake kwa kujitolea bila ya kugeuka nyuma, kwani ana imani Mungu yupo na anatenda muujiza kama alioutenda kwake.


"Unajua mimi katika maisha yangu hakuna ninayemwamini zaidi ya Bwana Yesu, kwa kuwa bila ya yeye mie nisingekuwa hapa nilipo, kwa taarifa yenu wapendwa mimi nilishakuwa dereva taxi, nilishakuwa kondakta wa daladala, lakini Mungu ni mwema na anatenda muujiza mpaka mimi kuwa hivi," alisema Msama.

Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, aliongeza kuwa hata hivi karibuni katika ajali aliyoipata akienda Dodoma licha ya kupinduka gari mara nne lakini alitoka akiwa hai.

Harambee hiyo iliyoenda sambamba na mnada, ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili kama Masanja Mkandamizaji, Edson Mwasabwite aliyeimba wimbo wa Ni kwa neema tu.

Mbali ya kiasi hicho alichotoa, Msama pia alichangia katika mnada uliofanyika katika tamasha hilo na kununua mtungi wa gesi kwa sh. laki 5.

No comments: