MKURUGENZI MKUU ATEMBELEA ENEO LA KUCHIMBUA MAJI KWA AJILI YA SAFARI CITY

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiwasili katika eneo la shamba la Magereza patakapochimbuliwa maji kwa ajili ya mji mpya wa Safari City jijini Arusha hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipata maelezo panapo alama ya kisima cha kwanza kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Arusha, James Kisarika aliyeambatana na watendaji wake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipata maelezo panapo alama ya kisima cha kwanza kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Arusha, James Kisarika aliyeambatana na watendaji wake. 
 Meneja na watendaji wake alimwonyesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu umbali kati ya Safari City na eneo hilo. Ni karibu Kilometa 2.5.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipata maelezo kuhusu visima hivyo kuwa vitakuwa vitatu na kwa pamoja vitaweza kusukuma zaidi ya lita 1,000,000 kwa siku.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akionyeshwa tanki la kiwanda cha A TO Z cha kutengeneza vyandarua vya mbu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo. Aliagiza hatua za kuanza kwa uchimbaji na usukumaji maji Safari City zianze mara moja sambamba na maandalizi ya kuanza kwa ujenzi. Pia alimshukuru sana Kamishina Mkuu wa Magereza kwa kutoa kibali.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu pamoja na Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Arusha wakiangalia mandhari ya eneo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiondoka katika eneo la tukio akiwa amefurahia hatua ilizofikiwa kwa upatikanaji wa maji.  

Comments