Friday, September 26, 2014

VIONGOZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MKOANI KATAVI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

KamViongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo   (CHADEMA)  Mkoa wa Katavi   na wafuasi wake 16 wa  wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahari Kidavashari  alisema kuwa viongozi hao walikamatwa  Septemba 25,majira ya saa 11.30 asubuhi mtaa wa majengo mkabala na nyumba ya kulala wageni ya Dubai Kata ya Kashaulili Wilayani Mpanda.
 Viongozi hao na waafuasi wao walikamatwa baada ya kufanya  Maandamano bila kibali   kwa ajili ya kuunga mkono maagizo yaliyotolewa na Viongozi wao wa Kitaifa ya kufanya maandamano  nchi nzima  kwa lengo la kuishinikiza Serikali isitishe  Kikao  Maalumu cha Bunge la Katiba  na kusitishwa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Wanaoshikiliwa na  Polisi ni Almasi Ibrahim Ntije Katibu wa Chadema  wa Mkoa wa Katavi, Abrahma Mapunda (16),Mwenyekiti wa Chadema  wa Wilaya ya Mpanda,Hamisa Kolongo (60) Katibu wa Chadema Mpanda.
  Wengine waliokamatwa ni Lameck Constantino (37) Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mpanda na Mkazi wa Itenka, Mlokozi Bagasheki (30) Mwenyekiti wa Vijana Cretus Aloyce (320Katibu wa Jimbo la Mpanda na Shabani Ibrahimu (26)Katibu wa Vijana Chadema na mkazi wa Kotazi.
Mbali ya viongozi hao pia wafuasi wengine waliokamatwa ni Kenedy Zakayo (20) mwanachama mkazi wa kijiji cha Ilebula,Mariam Omary (43)Katibu muenezi  wa Chadema, mkazi wa majengo,Fransisco Misigalo (29) mwenyekiti wa vijana Mkoa Mkazi wa Kashaulili,Selemani Hamisi (25) mkulima wa misunkumilo.
Wengine waliokatwa ni Anselemu Kanyengele (45) mkazi wa Majengo, Kasena Maulid Mjumbe wa Chadema Wilaya,Mwailwa James (35) mwanachama na mkazi wa kotazi, Emil Kalomo(30) mkulima,na Seif Ibrahimu(34) mwanachama na mkazi wa Majengo.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa viongozi wa chama hicho walieleza kuwa awali  Chama hicho kiliandika barua  hapo Septemba 22 kwa jeshi la polisi wakiomba kufanya maandamano tarehe 25 pamoja na Mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mpanda Hoteli
 Hata hivyo barua hiyo ilijibiwa na   jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda hapo  Septemba 24  ikikitaka Chama  kisifanye Maandamano wala Mkutano wa hadhara.
Kwa mujibu wa Maelezo ya  Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda  Idd Faraja alieleza kuwa   Chama  kiliamua  kufanya maandamano hayo baada ya kufanya maandalizi ya maandamano  hayo  na jeshi la polisi  kuchelewa  kuwapatia barua ya  kuwazuia kufanya maandamano na mkutano.
 Akaeleza kuwa  kitendo cha Jeshi laPolisi kuchelewa kujibu barua yao ya kuomba kibali  walivyoona  imekuwa kimya walijijua kuwa wamekubaliwa.wakaamua kufanya maamuzi ya kuandamana bila kibali.
 Katika Hatua nyingine Ofisi za Chadema  ambazo zipo katika Mtaa wa Majengo  A’ jana kutwa nzima zilishinda zimezungukwa na Askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa na silaha chini, PIA  Kituo Kikuu cha Polisi  Wilaya ya Mpanda  kiliimalishwa kwa Ulinzi baada ya kuwepo ulinzi kuhofiwa kuvamiwa  na  wafuasi wa Chadema  walioonekana kuwa na hasira.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahari Kdavashari amewatahadharisha wananchi na wakazi wa Mkoa huo wa Katavi kutojihusisha na maandamano ya namna yeyote ya Kisiasa  hadi hapo yatakaporuhusiwa.
Pia amewaasa kutoshawishiwa na chama chochote kushiriki maandamano au migomo kwani watakuwa wamekiuka sheria na taratibu za nchi. 

No comments: