KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA TAARIFA KUHUSU AWAMU YA PILI YA KAMPENI YA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI-KAMPENI GOGOTA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
Mratibu wa Dawati la Katiba LHRC, Anna Henga 
Mwanasheria wa LHRC,  Harold Sungusia
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni Gogota). Kulia ni Mratibu wa Dawati la Katiba wa kituo hicho, Anna Henga na Mwanasheria wa Kituo hicho, Harold Sungusia. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu 0712-727062)
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu kimedai kuwa Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea linaendeshwa kimabavu kwa na kutumia fedha za wananchi bure wakati wakijua fika hakuna katiba itakayopatikana.
 
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadam (LHRC) Dk. Helen Kijo-Bisimba, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni gogota) kwa wananchi.
 
“Cha kusikitisha ni kwamba tumepoteza mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kusaidia kwenye sekta mbali mbali zikiwemo za afya na elimu kwa kuwalipa wajumbe wa bunge la katiba,” alisema.
 
Alisema wakati wa kampeni hiyo ambayo imefanyika kwenye mikoa 20 nchini kituo hicho kimebaini kuwa wapo asilimia kubwa ya wananchi wanakerwa na mwenendo wa mchakato wa bunge hilo kwa kuchakachua maoni yao yaliyokusanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba.
 
Alisema wakati wa kampeni hiyo ya gogota kituo hicho kimefanikiwa kufika kwenye wilaya zote, na kata tatu kwa kila mkoa ambapo kilifanikiwa kurudisha ajenda ya katiba na uelewa wa rasimu ya pili ya katiba kwa wananchi.
 
Alisema hiyo ni moja ya mafanikio waliyoyapata kuyajua kwa wananchi kwenye kampeni hiyo ambayo ililenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika mchakato hususani kufuatilia bunge la katiba na upigaji wa kura ya maoni muda utakapo fika.
 
Pamoja na mafanikio hayo pia kitu hicho kimekutana na changamoto mbali mbali ikiwemo ya uelewa mdogo kuhusu katiba hususani walio pembezoni mwa miji.
 
Alitaja mikoa hiyo ni Arusha, Tanga, Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mbeya, Rukwa, Kilimanjaro, Manyara, Katavi, Iringa, Mara, Njombe, Ruvuma, Pemba Kaskazini, Kusini, Pemba mjini Magharibi, Unguja Kusini na Kasazini.
 
Alitaja changamoto nyingine ni kutokujua kusoma na kuandika kwa baadhi ya wananchi, umangi meza kwa badhi ya viongozi wa mikoa, hofu ya kutopata katiba na mfumo dume kwenye jamii.

Comments