Friday, September 26, 2014

HALMASHAURI YA MPANDA YAKAMILISHA UJENZI WA MAABARA KWA ASILIMIA 100

KIBIRIT.Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya.Mpanda Yasini Kibiriti akifungua kikao cha Baraza la Madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.???????????????????????????????Diwani wa Viti Maaalum Tarafa ya Mwese inayojumisha Kata za Kapalamsenga Ikola na Karema yenyewe akichangia kwenye kikao cha Madiwani wakati wa kikao hicho wengine ni madiwani wa Halmashauri hiyo.
………………………………………………………………………….
Na Kibada Kibada-Katavi

Zaidi ya shilingi milioni 80 zimetengwa na  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya maabara ya Sayansi vilivyojengwa katika shule za  Sekondari  zilizoko kwenye  Halmashauri hiyo.
Hayo yamelezwa na Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Yasini Kibiriti wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza  la Madiwani  kwa mwaka 2014/2015 kilichofanyika  kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halamsahuri hiyo.
Akizungumza katika Kikao hicho Mwenyekiti Kibiriti ameeleza ujenzi wa maabara kwa Halmashauri ya Mpanda uko vizuri sana  kwani wameishakamilisha ujenzi na fedha hizo zilizotengwa ni kwa ajili ya ukamilishaji ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vitakavyotumika kwenye nmaabara hizo.
Akaongeza kuwa hadi kufikia oktoba 15 mwaka huu anaimani watakuwa wamekamilisha kila kitu na kwa Halmashauri za Mkoa wa Katavi Halamshauri ya Mpanda inaonekana kufanya vizuri katika ukamilishaji wa ujenzi wa maabara ingawa haipongezwi kwa juhudi inazozifanya katika kutekeleza kwa wakati maagizo yanayotolewa na Viongozi wa juu  wa serikali  kuanzia ngazi ya Mkoa na Taifa.
Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  aliagiza ujenzi wa Maabara kwa shule zote za sekondari   na ifikapo mwezi novemba mwaka huu kila Halmashauri iwe imekamilisha ujenzi huo,akawagiza wakuu wote wa Wilaya na Mikoa ambao hawatakamilisha ujenzi wajiondoe wenyewe kwa upande wa   Halmashauri ya Mpanda wao wamefanikiwa kukamilisha ujenzi huo.
Katika ujenzi huo  zaidi ya shilingi milioni 560 zimetumika kujenga maabara nane zenye vyumba viwili viwili  kwenye shule za Sekondari Mpandandogo,Karema,Ilandamilumba,Ikola,Mwese,naMishamo maabara zote hizo ziko vizuri kweli kweli tofauti na inavyozungumuziwa na watu kuwa Halmashauri iko nyuma katika utekelezaji wa ujenzi wa maabara siyo kweli.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Estomih Chang’ah alieleza changamoto inayoikabili Halmashauri katika utengenezaji wa barabara za Halmashauri hiyo kutokana na wakandarasi kutokuwa na Vifaa vya kutosha hali inayofanya ucheleweshaji wa kukamilika kwa barabara kwa wakati.
Chang’ah akaeleza wakandarasi wengi wanapokuja kuomba kazi kwenye Halmashauri hawakamilishi kazi zao kwa wakati ,ambapo wanatakiwa kutekeleza kazi zao kwa wakati lakini ajabu bado unakuta wanaomba msaada wa kusaidiwa vifaa vya ujenzi wakati walishapatiwa kazi  kwa mjibu wa mkataba wanatakiwa wakabidhi kazi siyo kuomba msaada tena wakusaidiwa vifaa vya kukamilishia kahiyo kule waliko pewa kazi.
Wakiongea katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Kapalamsenga Moses Joseph alieleza kuwepo ucheleweshaji wa kusambaza kifusi kwenye barabara ya Kapalamsenga Ifume kazi inayofanywa na mkandarasi ambaye  aliingia mkataba na Halmashauri lakini kazi hiyo inaonekana kusuasua na haifahamiki lini ataikamilisha.

No comments: