BAADA YA SHULE YA SEKONDARI YA IFUNDA TECH KUFUNGWA KWA VURUGU UONGOZI WA SHULE HIYO WAWAITA WANAFUNZI 28
Mkuu wa shule ya sekondari ya Ifunda Tech akizungumza na wanafunzi hao hivi karibuni
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ifunda Tech
Uongozi wa shule ya sekondari ya Ifunda tech wilaya Iringa mkoani Iringa imewaita wanafunzi 28 kufika shuleni hapo octoba 2 ikiwa ni baada ya shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana kutokana na wanafunzi hao kufanya vurugu kubwa hivi karibuni .
Hatua ya uongozi wa shule hiyo kuwaita wanafunzi hao imekuja zikiwa ni zaidi ya siku 4 kupita toka shule hiyo kufungwa kufuatia vurugu kubwa shuleni hapo na kusababisha hasara kubwa ya mali za shule hiyo
Makamu mkuu wa shule hiyo Ernest Sakafu ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na mtandao wa matukio daima ofisini kwake .
Amewataja wanafunzi wanaotakuwa kufika shuleni hapo kuwa ni steven Nyiriri,petro Kalolo, Iddi shaban, John Zephania, Edwin Rwegoshora, Adinan Mrisho Mtiti, Izengo Dotto, Gaspar Manyagi, Shemson Amoni, Halid Omari, Said Sambo, Paschal Lusukanija ,Fred Kidava na Eliji Nguvila.
Wengine ni Stambuli Daluweshi, Jackson Mlowe, Sidi Kayombo, Yusuph Makale, Joseph Antony, Allan Laurent, Rose Kayombo, Enoce John, Rashid Kandoro, Abdul Zumo, Petro Silwimba, Joyce Nestory, Michael Kimario na Athuman Ahamad.
Alisema kuwa kwa sasa shule hiyo imefungwa kutokana na vurugu hizo hivyo shule hiyo itafunguliwa wakati wowote kuanzia sasa.
Comments