Monday, September 29, 2014

Hafla ya Chakula cha jioni kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund yafana jijini Dar


 Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund, Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kuendesha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.
 Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa akitoa hotuba yake kwa wageni wa mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.Picha zote na Othman Michuzi.
 Katibu wa Bonnah Education Trust Fund,Mary Muwasa akizungumza machache ikiwa ni pamoja kuwatambulisha wadhamini mbali mbali waliojitolea ili kufanikisha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
  Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa
Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. BRamadhan Madabida (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 8 kutoka kwa Mwenyekiti wa GCUT Group Tanzania,Lucy Jeremiar Gilya.Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg.
Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 15 kutoka kwa Meneja wa Miles Networks International nchini Tanzania,Diana Paul (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg.
Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 4.4
kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Resolution Insurance,Angela Tungaraza (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg.
Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 9.8
kutoka kwa Meneja Uajiri wa Kampuni ya Aramex Tanzania,Jane Stella Njagi (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
 Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg.
Ramadhan Madabida akiendelea kutoa hotuba yake.
 Meza Kuu.
 Mshehereshaji katika hafla hiyo,alikuwa si mwingine bali Mdau Ephrahim Kibonde.
Baadhi ya wageni waliohudhulia hafla ya ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund wakifatilia kwa makini harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

No comments: