Naibu Mkuu na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Li Xuhang akizungumza na raia wa China wanaoishi Tanzania na wananchama wa Chama cha Wachina Tanzania juu ya kufuata sheria za Tanzania na China.
Naibu Mkuu na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Li Xuhang (kulia) akizungumza na raia wa China wanaoishi Tanzania.
Lin Zhiyong Mkuu wa Wakikilishi wa Masuala ya Kiuchui na Kibiashara katika ubalozi wa China nchini Tanzania akizungumza na raia wa nchi yake wanaoishi Tanzania.
Baadhi ya raia wa China wanaoishi Tanzania wakiwasikiliza viongozi wa ubalozi wa nchini hiyo (hawapo pichani) baada ya wenzao kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini kwa tuhuma za kufanya magendo ya meno ya tembo.
---
Hussein Makame, MAELEZO
CHINA ina shirikiana na Tanzania kufanya uchunguzi wa tuhumu zanazowakabili raia watatu wa nchi hiyo wanaodaiwa kukamatwa wakiwa na meno ya tembo 706 jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Li Xuhang wakati alipozungumza na wanahabari kwenye ubalozi wa nchi hiyo kwenye mkutano wa Chama cha Wachina Tanzania uliofanyika kwenye ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Alisema kuwa Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing pamoja na ubalozi wake wanalaani vikali kitendo hicho cha mauaji ya tembo na magendo ya meno yake na kwamba nchi hiyo iko tayari kushiurikiana na Tanzania kupambana na wahalifu.
Aliongeza kuwa Serikali ya China inaiunga mkono kwa dhati Serikali ya Tanzania kipingana na magendo ya meno ya tembo na Jeshi la Polisi lake linapenda kushirikiana na Jeshi la Polisi la Tanzania kupambana na wahalifu.
Alifafanua kuwa ubalozi huo umestushwa na habari hiyo iliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini na kwamba sasa upande wa China unafanya uchunguzi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kupata uhalisia wa habari hiyo.
“Jana na leo tumepeleka Maafia wa Ubalozi wetu kuchunguza kwanza kuthibtisha utambulisho na pia tumeliambia Jeshi la Polisi kwamba hawa watu watatu kkama ni raia wa China haki zao za msingi lazima zilindwe”, alisema Xuhang.
Aliongeza kuwa “Tumeamua kufanya uchunguzi wa kina kwa sababu hatuwezi kufanyia kazi taarifa za vyombo vya habari, hivyo lazima tuthibitishe taarifa hizi na ikiwa ni za kweli tutakuwa tayari kuisaidia Serikali ya Tanzania kuwafikisha mahakmani wahusika”
Alifafanua kuwa kufanya magendo ya meno ya tembo ni kosa kubwa la jinai kwa nchi ya China na adhabu kali inatolewa kwa mtu anayepatikana na kosa hilo ikiwemo itakutwa na kilo sita za meno hayo anafungwa jela miaka kumi au zaidi.
“Ikiwa utapatikana na hatia ya meno ya tembo ya zaidi ya kilo sita unaweza kuhukumiwa jela miaka zaidi ya kumi au kunyongwa kabisa, kwa hiyo Serikali ya China inaongoza duniani kwa kutoa adhabu kali kwa kosa hilo” alisema Xuhang.
Aliwataka raia wote wa China wanaoishi Tanzania kufuata Sheria za China na za Tanzania na kwamba wasifanye kitendo chochoe kinachokwenda kinyume na sheria kama vile kufanyamagendo ya meno ya tembo.
Comments