Thursday, November 14, 2013

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEAO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MHE. UMMY MWALIMU AFUNGUA KIKAO KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA DEMOKRASIA KATIKA NGAZI ZA CHINI KWA MTIZAMO WA KIJINSIA

 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifungua kikao cha majadiliano ya taarifa juu ya Utafiti Kuhusu Hali ya Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa kijinsia
 Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe. Ibrahimu Lipumba akitoa taarifa za Awali za Matokeo ya Utafiti huo. Mhe.Lipumba amesema Utafiti huo ulihusisha madodoso mia sita(600) kutoka katika Mikoa minane nchini
Baadhi ya Washiriki wa kikao wakati wa majadiliano Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF)Profesa Ibrahimu Lipumba. Picha zote na Asteria Muhozya-Wizara ya Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto
--- 
Naibu Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefungua kikao cha Kujadili Matokeo ya Utafiti wa Hali ya Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa Kijinsia.

Kikao kimeandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini kwa ushirikiano wa Shirika la Kimataifa la IDEA, na kuvishirikisha  Vyama vya siasa, Wizara, Halmashauri na  Baadhi ya Taasisi Zisizo za Kiserikali.Kuijadili taarifa hiyo.

 Wakati akifungua kikao Mhe.Ummy amesisisitiza kuwa, Demokrasia kamili haiwezi kupatikana bila ushiriki sawa wa wanaume na wanawake na kuongeza kuwa, Serikali za mitaa ni wadau wakubwa wa kuleta usawa wa demokrasia.

No comments: