Friday, November 01, 2013

Waziri Nahodha aongoza wanajeshi, wakazi wa Dar kuaga mwili wa afisa wa jeshi la Tanzania Luteni Mlima aliyefariki Congo- DRC


    Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakishusha kwenye gari jeneza lenye mwili wa  askari mwenzao, marehemu Luteni Rajab Mlima wakati wa maziko yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam jana jioni Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima Gavana eneo la Goma.
   Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakiwa wameinamia kwa huzuni  jeneza lenye mwili wa  askari mwenzao, marehemu Luteni Rajab Mlima wakati wa maziko yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam jioni hii. Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima Gavana eneo la Goma.
  Waombolezaji wakijiandaa kufanya maziko
  Waombolezaji wakifanya maziko
  Askari wa JWTZ wakitoa heshima wakati wa maziko

No comments:

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Awasili Marekani kwa Kikao cha UNGA 80

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango , leo tarehe 21 Septemba 2025 amewasili jijini New York, Marekani . ...