Thursday, November 21, 2013

ALIYEKUWA RAIS WA BOTSWANA MH. FESTUS GONTEBANYE MOGAE AMTEMBELEA RAFIKI YAKE MH. MOHAMMED DEWJI‏

 Mwenyekiti wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji akibadilishana mawazo na aliyekuwa Rais wa Botswana Mh. Festus Gontebanye Mogae alipomtembelea rafiki yake Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) ofisini kwake.
Mh. Mohammed Dewji katika picha ya pamoja na aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae.
Mwenyekiti wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji kwenye picha ya kumbukumbu na aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus GontebanyeMogae.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group Mh. Mohammed Dewji siku ya jana alipata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake, aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae. Mh. Mogae ambaye pia amewahi kuwa mshindi wa tuzo ya Mafanikio katika Uongozi itolewayo na mfanyabiashara mzawa wa Sudan Bwana Mo Ibrahim mwaka 2008, alikuwa na mazungumzo binafsi na Mohammed Dewji (Mo) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar-es-salaam.
Tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, humuwezesha mshindi kupata kitita cha dola za Kimarekani millioni 5, na dola za Kimarekani 200,000 kila mwaka kwa maisha yake yote. Hizi ni baadhi ya picha, zilizopigwa na mpiga picha wetu, jana kwenye ofisi za MeTL Dar-es-salaam.

No comments: