WAZIRI DK.NCHIMBI AZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITATU WA KUBORESHA MADAWATI YA KIJINSIA NA WATOTO NDANI YA JESHI LA POLISI
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova alipowasili kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova. Kushoto ni Wanamawasiliano kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu na Sangita Khadka.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kuwasilia eneo la tukio.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema (kushoto) na Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova wakati wakielekea jukwaa kuu.
Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan (katikati) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kushoto) Kulia ni Mkuu wa Mabalozi wa EU nchini Filiberto Sebregondi.
Pichani juu na chini Maandamano yakiwasili kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
Taasisi mbambali zikiwa zimebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kutokomeza ukatili wa Kijinsia.
Burudani kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa Askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali pamoja na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan akizungumza kwa niaba ya nchi yake ambapo amesema Ireland itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa ukaribu zaidi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizindua kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou, wapili kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimshukuru Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou mara baada ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi ulio chini ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuzindua ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Kipolisi Temeke. Kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi.Waziri Nchimbi katika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali baada ya waziri huyo kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akiteta jambo na mmoja wa maafisa wa Jeshi la Polisi mara baada ya uzinduzi huo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa redio wa BBC. Katikati ni Afisa Habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Usia Nkhoma Ledama.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini, Dr. Alberic Kacou mara ya uzinduzi.
Comments