
Aliyekua Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Ananilea Nkya
----
Vijana Dr Kitila na Zitto.
Nimesoma matamko yenu mliyoyatoa jana.
Nakupongezeni maana mmeonyesha kwamba mnatambua ninyi ni binadamu na si malaika.Mmetuonyesha sisi wananchi kwamba ninyi ni wanasiasa wenye hofu ya Mungu. Mmetuonyesha kwamba mmeamua kutoa maisha yenu kuwatumikia Watanzania na si kwa maslahi yenu binafsi au maslahi ya chama chenu CHADEMA pekee, bali maslahi ya Watanzania. Mmeandika historia mpya inayotoa mafunzo mbali mbali.
Ninachowashauri na hiki narejea nilichokiandika kwenye uzi uliokuwa na tamko la Zitto ni kwamba muendelee kusimama imara na chama chenu bila kinyongo chochote kutokana na yaliyotokea mkiwa na lengo moja kupigania maslahi ya umma mpana ili NCHI YETU ISHINDE. Aidha, CHADEMA kama chama makini cha siasa, muendelee kuangalia mbele kwa umakini sana muwashinde wenye nia chafu dhidi yenu. Na ushindi wenu utatokana na nia yenu safi kwa nchi yenu na watu wake, umoja wenu, umakini wenu, usafi wa matendo yenu, kuheshimiana kwenu kwenu ninyi kwa ninyi kuonyana ili kurekebishana na kisha kusameheana kwenu.
Siku zote mkumbuke, thawabu yenu kuu kama wanasiasa itatokana na jinsi siasa za chama chenu zitakavyofanikisha kuijenga Tanzania mpya isiyo na kiwango kikubwa cha rushwa kama ilivyo sasa, isiyo na ubaguzi wa haki kama ilivyo sasa kwamba baadhi ya viongozi hata wakituhumiwa kutenda jinai kubwa mkono wa sheria hauwezi kuwadaka haraka la bda kwa shinikizo ili hali mwananchi wa kawaida akiiba hata ugali anaweza kuishia jela wiki inayofuata .
Kadhalika Tanzania mpya yenye hospitali nzuri zenye vifaa, madawa na madaktari (naamini Dr Sengondo Mvungi asingekufa kama tulikuwa na hospitali nzuri hapa yenye vifaa na madawa madaktari wangemuwahi), shule nzuri na Tanzania mpya isiyo na pengo kubwa la kipato kati ya vwanasiasa na watumishi wengine wa umma n.k.
Nawatia shime wote mnaopigania wananchi na Mungu awabariki sana.
By the way you kijana Samsoni Mwigamba sikusoma tamko lake yeye kasemaje?
Ananilea Nkya E-mail:ananilea_nkya@yahoo. com
No comments:
Post a Comment