MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI , ABSALOM KIBANDA AANGUA KILIO UKUMBINI KABLA YA KUKABIDHIWA TUZO





Kibanda akielekea  kupokea  tuzo huku akila kwa uchungu


Kibanda akibembelezwa na mmoja kati ya majaji  wa tuzo hioy
Mgeni  rasmi katika hafla  hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi Bw  Tido Mhando  wa tatu  kulia  akimkabidhi mshindi  mfano  wa hundi ya Tsh milioni 10,  katikati ni mjane  wa Mwangosi  Itika Mwangosi  wa kwanza  kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanji na  rais  wake  Keneth Simbaya
Na  Francis Godwin Blog Mwanza
Tukio  hilo ambalo ni la kwanza katika  histori  ya  washindi wa tuzo mbali mbali kutokea nchini  limetokea leo katika Hotel la JB jijini Mwanza  wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hiyo iliyotolewa na UTPC.
Kibanda ambae muda  wote  alionekana kutulia katika nafasi yake hadi pale jiji mkuu wa tuzo hiyo mwanahabari maarufu nchini Tanzania Hamza kasongo kupita mbele na kusoma  sifa  za mshindi wa tuzo  hiyo na kumwita  mmoja kati ya majaji  kutaja  jina la mshindi .
Baada  ya  kibanda kutangazwa mshindi hakuweza kuonyesha furaha kama ilivyo kwa washindi  wengine na badala yake kuanza  kulia kwa uchungu kiasi cha baadhi ya wajumbe ukumbini hapo akiwemo makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanjo kuungana nae  kuangusha  chozi  ukumbini hapo na kufuatiwa na wajumbe mbalia mbali akiwemo mjane wa Mwangosi Bi Itika Mwangosi  .
Kutokana na hali hiyo zoezi hilo lilisogezwa  mbele na kupigwa  wimbo maarum wa  kumkumbuka Mwangosi na baada ya hapo Kibanda alikaribishwa  kukabidhiwa  tuzo yake.
Hata  hivyo Kibanda  alionyesha  kuwa na simanzi nzito na hata  kuueleza  umma uliokuwepo hapo kuwa tuzo hiyo inamtia majonzi zaidi kwa kukumbuka kifo  cha Mwangosi na yale  yaliyomkuta yeye kwa kuvamiwa na kutoborewa  jicho lake .
Hivyo alisema mbali ya kesio hiyo kuendelea  kuzunguswa bado yote anamwachia Mungu aliyemfanya kuwa hai hadi leo na kuwa katika fedha  alizopata  za tuzo  asilimia 10 atamrejeshia  mwenyezi Mungu na fedha inayobaki  atagawana  nusu kwa nusu na mjane wa Mwangosi
wakati huo  huo wanahabari  nchini  wametakiwa  kujenga  umoja katika  kupinga sheria  kandamizi  ya  vyombo  vya habari  na  wanahabari nchini inayatarajia  kupitishwa na  wabunge wa  bunge la jamhuri ya  muungano wa Tanzania.
Meneja  wa uthibiti  wa ubora  kutoka  baraza la habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike ametoa  kauli hiyo  leo  jijini Mwanza wakati  wa hafla  ya  kukabidhi tuzo  ya  kishujaa na uandishi  uliotukuka  ya  Daudi Mwangosi .
Mtambalike  amesema  kuwa  idadi ya  waandishi  kutekwa na kuuwawa  imezidi  kuongezeka  hapa nchini  huku kasi  ya  serikali  kuvifungia vyombo  vya habari  pia  inaendelea  kuongezeka .
Hivyo iwapo wanahabari  nchini  hawataungana  katika  kupinga  manyanyaso  dhidi  ya  vyombo vya habari na  kupinga  sheria  kandamizi  dhidi ya  vyombo  vya habari na wanahabari suala  la uhuru  wa  vyombo  vya habari nchini  litaendelea  kubaki ndoto.

Comments