Monday, November 18, 2013

Bunge lakataa kubariki ‘Division 5’



Mwenyekiti Wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii  Magreth Sitta
----
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, imevikataa viwango vipya vya alama za ufaulu kwa elimu ya sekondari vilivyotarajiwa kuanza kutumika mwaka huu na kutaka utaratibu na alama zilizotumika mwaka jana, zitumike kupanga matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa mwaka huu.

Serikali ilitangaza utaratibu mpya wa alama za Mitihani ya Kidato cha Nne na Sita kwa kufuta Daraja la Sifuri na kuleta Daraja la Tano.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stephen Ngonyani  alisema jana kuwa kamati hiyo ilichukua uamuzi huo kwa kuwa pamoja na udhaifu ulio kwenye alama hizo, kamati yao haikuhusishwa katika mchakato wa kuandaa alama hizo. 
“Mwenyekiti wangu (Margaret Sitta) alisema kile hakiwezekani, kuna viwango ambavyo wameleta havipo kwenye nchi nyingine duniani, tumewaambia wakavifanyie kazi walete tena,” alisema mbunge huyo wa Korogwe Vijijini, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Profesa Maji Marefu.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.........

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...