Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa vijana waendesha pikipiki mjini Mbinga ambao unafadhiliwa na mbunge wa jimbo la Mbinga Mh Gaudence Kayombo, uzinduzi huo umefanyika kwenye mkutano wa hadhara ulioafnyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Mbinga, Kinana yuko katika ziara ya mikoa mitatu Ruvuma, Mbeya na Njombe akiongozana na Dr.Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. akikagua miradi ya maendeleo na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ikiwani pamoja na kuimarisha uhai wa chama, Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Mbinga Gaudence Kayombo na kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha waendesha pikipiki wa Mbinga Al Haji Mussa Ramadhan(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBINGA) Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mwenyekiti wa shina katika kijiji cha Amani Makolo wakati alipowasili katika jimbo la Mbinga leoKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka kulia akiongoza viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya Mbinga katika kilimo kwenye shamba la akina mama na vijana wa mjini Mbinga walioanzisha umoja wao kwa kuanzisha kilimo cha alizeti wakisaidiwa na Mbunge wao na Mkuu wa Wilaya, Shamba hilo lina ekari 500 na kwa sasa wameshalima hekari 100 na wanaendelea na upanuzi wa kilimo katika shamba hilo ambalo wameazimwa na Jshi la MagerezaNape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa kwanza waliovaa mashati ya kijani akiwa amekaa na wanachama wa CCM katika kijiji cha Amani Makolo leo.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Nape Nnauye waliopanda pikipiki wakijaribu kuziwasha pikipiki hizo mara baada ya kuzindua mradi huo wa vijana mjini Mbinga.Wana CCM wa Kijiji cha Amani Makolo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza naoWana CCM wapya wa Amani Makolo wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama.Nape Nnauye akifurahia jambo na Bibi Dafroza Luoga wakati alipokuwa wakizungumza mawili matatu na bibi huyo.Wananchi wa kijiji cha Amani Makolo wakifurahia ghala lao la kuhifadhia mahindi mara baada ya katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kukagua ghara hilo.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mtunduwalo Wilayani Mbinga. 4tKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Tarn Brereton Mtendaji mkuu wa kampuni ya TANCOAL inayomiliki mgodi wa Makaa ya mawe wa Mangaka Wilayani Mbinga wakati alipotembelea mgodi huo kushoto ni Gideon Nasari Mkurugenzi Mkuu wa NDC.Mitambo mbalimbali inayofanya kazi ya kuchimba makaa ya mawe kwenye mgodi wa Mangaka.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mgodi huo leoHapa ndipo kwenye mtambo wa kusaga makaa hayo.Dr. Asha Rose Migiro na Nape Nnauye wakisalimia wananchi wakati msafara huo ukiwa njiani kuelekea Mbinga.Msafara ukielekea MbingaVijana na akina mama na vijana wa Mkwaya kata ya Kilimani wakiendelea na shughuli za kusafisha shamba lao lililopo nje kidogo ya mji wa Mbinga,Mtangazaji wa TBC Gerson Msigwa akishiriki katika kilimo shambani KilimaniKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana na akina mama wenye umoja wao wanaolima shamba hilo wakati alipokagua shamba hilo.Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa Mbinga katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini MbingaKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbinga katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Mbinga
Comments