Waziri Dr Emmanuel Nchimbi ateua Bodi ya Shirika la uzalishaji mali la Polisi

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
 Kutokana na Maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi kumekuwepo na mikakati mbalimbali  inayolenga uboreshaji wa miundombinu yake, ikiwa ni pamoja na kupata ofisi, vituo vya polisi, makazi ya kuishi askari makambini, vifaa na vitendea kazi ili kuimarisha ulinzi na usalama nchini.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi iliona kuna umuhimu  wa kuanzisha Shirika la uzalishaji mali la Polisi (Tanzania Police Corporation Sole) ili kuendelea kufanikisha malengo  ya maboresho yanayoendelea.

Kufuatia hatua hiyo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliridhia kuanzishwa kwa Shirika la Uzalishaji  ndani ya Jeshi la Polisi baada ya kusaini Amri ya uanzishwaji Shirika hilo tarehe 27/9/2012 kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1974 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2000.

Mara  baada ya kusainiwa na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kwa mujibu wa sheria ameteua Bodi ya Shirika hili  na kumteua Ndugu EMMANUEL HUMBA kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa miaka mitatu kuanzia tarehe 19/9/2013, aidha amewateua wajumbe wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi hiyo:-

(1)Mwakibinga E.P.M Mihalale- Msajili wa Hazina Msaidizi

(2)Jehad Abdallah Jehad –Msajili Bodi ya Wakadiriaji na Wasanifu
   Majengo

(3) Melkior Temu- Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

(4) T.M.E Andengenye –DCP Mkuu wa Utawala Jeshini 

(5) A. Nyamhanga –ACP-Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Bajeti Jeshi la
Polisi

(6)Samwel Marco-Meneja Hazina –(Tressure)-TIB

(7) John Mathew- Kaimu  Mkurugenzi Mhamasishaji- TIC

Katika uteuzi huo amemteua pia DCP- SOSPETER M. KONDELA kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kwanza wa Shirika hilo.uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na
 Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
18 NOVEMBA, 2013.

Comments