Friday, November 01, 2013

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO ATEMBELEA WILAYA YA MBOZI IKIWA NI PAMOJA NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 Kikundi cha ngoma za asili kutoka katika kijiji cha Lyula kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya ugeni wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo katika kijiji hicho.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wanakijiji wa Lyula. Profesa Muhongo amewataka wananchi hao kujiandaa  mradi wa umeme unaotarajia kuanza kutekelezwa mapema Novemba kwa  kufunga nyaya za umeme katika nyumba zao.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiagana na wanakijiji wa Lyula. Wanakijiji hao wamefurahishwa mno na ujio wake huku wakitamani aendelee kuwa nao.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisikiliza kero ya mmoja wa wananchi wa kata ya Isansa.
 Wanakijiji wa kata ya Isansa wakishangilia hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)
Mmoja wa  wakazi wa kata ya Isansa akiimba shairi la kupongeza juhudi za  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo katika kupeleka umeme vijijini.

No comments: