WAZIRI WA ELIMU, DKT. SHUKURU KAWAMBWA ATEMBELEA BANDA LA ARUSHA TECHNICAL COLLEGE KWENYE MAONESHO YA KIMATAIFA YA MADINI JIJINI ARUSHA
Waziri wa Elimu, mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa akipokea Maelezo mafupi kuhusu Kozi ya Ukataji Madini na Utengenezaji wa Vito vya thamani kutoka kwa Bi. Shahzimin Premji alipotembelea banda la Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).
Waziri wa Elimu, Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea banda ya Arusha Technical College. Chuo hicho kinatoa mafunzo ya Uchakataji madini na kutoa wataalamu wanaokubalika katika soko.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Masika (Kushoto) alimkabidhi waziri wa Elimu, Dkt. Shukuru Kawambwa moja wa Vito vya thamani vilivyochongwa na wanafunzi wanaosoma Kozi ya Ukataji madini Chuo cha Ufundi Arusha.
Comments