Monday, November 04, 2013

LOWASSA ANGURUMA BUNGENI

Edward Lowassa.
Katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa nadra bungeni, Edward Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha kuweka vipaumbele vingi visivyotekelezeka kwa wakati.
Alitaka serikali kuweka nguvu katika vipengele vichache vya msingi kama ajira, afya, elimu na miundombinu.
Aliwapongeza mawaziri John Magufuli kwa kuimarisha barabara na Dk. Harrison Mwakyembe kwa kubuni mbinu za kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, alizosema zinachangia kuharibu uchumi kwani watu wengi wanakaa barabarani badala ya kufanya kazi.

Ameponda serikali kwa kutochukua maamuzi kwa wakati hali ambayo anaona inaleta matatizo katika Taifa. "ni lazima viongozi mchukue maamuzi magumu, siyo kila mtu analalamika, wananchi wanalalamika na viongozi pia wanalalamika hii haiwezekani>'

Alisema ili Serikali isonge mbele ni lazima ifanye maamuzi na kupunguza vipaumbele kubaki vichache kwani kwa sasa vipo vingi mno hali inayofanya visitekelezeke. "Vijana wanamaliza form four hawana ajira, wanamaliza darasa la saba hawana ajira, kule Ujerumani ........

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...