Wednesday, November 20, 2013

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUFUTA UMASKINI KWA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI

Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro alipotembelea wakati akianza ziara yake  katika Mkoa wa morogoro.
Katika ziara hiyo waziri Muhongo amesema Serikali ya CCM Imeamua Kutokomeza kabisa Umaskini na ndiyo maana inasambaza Nishati ya Umeme kwa kasi kubwa ili Nishati hiyo iwasaidie watanzania katika shuguli za uchumi ikiwemo Elimu,Viwanda na matumizi Mengine.Aidha Waziri Muhongo Amesema kuwa Kumekuwa na uharibufu Mkubwa wa Mazingira hali inayoashiria Jangwa kutokana na uvunaji wa miti kwajili ya Uzalishaji wa Mkaa na wameamua kusambaza Nishati ya Umeme kwa haraka ili kuiokoa nchi kuwa Jangwa.Waziri muongo ameongeza kwamba kwa sasa Bei ya kuwaunganishia wananchi umeme Imeshushwa Mpaka Shilingi 177,000/= tu kwa lengo la kuwawezesha watanzania wenye pato la chini kuunganisha umeme na kunufaika na Nishati hiyo.Pia waziri Muhongo ameongeza Shirika la Umeme wameagizwa kupokea Fedha kidogo kidogo kwa wananchi wote watakohitaji kuunganishiwa umeme na hawana Uwezo wa Kulipa fedha zote kwa Pamoja..
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Kushoto Akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris wakati walipompokea waziri wa Nishati na madini Mh Sospert Muhongo Mjini Morogoro
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris Kushoto akiwa na Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo kulia wakisikiliza taarifa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Iliyokuwa inasomwa na Katibu wa ccm Mkoa wa Morogoro hayupo pichani.
Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo Akiuliza jambo kwa Injinia wa shirika la umeme mkoa wa morogoro Ndugu Maro walipotembelea Kituo cha kuunganishia Umeme kilichopo Pangawe wakati wa ziara ya Waziri huyo ya Kukagua miradi ya kusambaza Umeme vijijini Mkoani Morogoro
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris Akifafanua Jambo katika ziara ya waziri huyo na kushoto ni Meneja Wa Tanesco Mkoa wa Morogoro Akisikiliza kwa makini
Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo Akipokelewa na Viongozi katika kata ya Mtamba Jimbo la Morogoro kusini lililopo Wilaya ya Morogoro Vijijini alipotembelea Wilaya Hiyo wakati akikagua Mradi wa Kusambaza Umeme vijijini Mradi Uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo La MCC.Waziri Muhogo Amesema Serikali ina nia ya kusambaza Umeme Vijiji vyote tanzania Ili kila mtanzannia afaidi  nishati hiyo..
Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo Akisaini Kitabu cha wageni kata ya Mtamba wilaya ya Morogoro Vijijini kabla ya kusikiliza kero za Wananchi wa wilaya hiyo kuhusu Umeme na uchimbaji wa Madini

Wananchi wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo

No comments: