Waziri wa Mambo ya Nje wa Usultani wa Oman, Mhe. Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Albusaidi, Novemba 9, 2026 amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Albusaidi amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Albusaidi atashiriki kama Mgeni Maalumu katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent Commission – JPC), unaofanyika kisiwani Zanzibar.







No comments:
Post a Comment