Balozi Irene Kasyanju Akutana na Afisa Msimamizi wa Mahakama iliyorithi shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ya mjini Arusha. Bw.Samuel Akorimo
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akisalimiana na Bw. Samuel Akorimo, Afisa Msimamizi wa Mahakama iliyorithi shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ya mjini Arusha. Bw. Akorimo alifika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mahakama hiyo na Wizara. Wanaoshuhudia ni Bw. Tiyarijana Mphepo, Afisa alifyefuatana na Bw. Akorimo na Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje.
Balozi Kasyanju akizungumza na Bw. Akorimo huku Maafisa wakinukuu mazungumzo hayo.
Bw. Akorimo akizungumza na Balozi Kasyanju kuhusu majukumu ya Mahakama hiyo.
Bw. Akorimo akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Wizarani huku Bw. Mphepo akishuhudia.Picha na Reginald Philip
Comments