KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, MINJA AMVISHA CHEO CHA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA MAGEREZA AFISA MWINGINE ALIYEHUDUMU ULINZI WA AMANI DARFUL

 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akimvisha Cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge ambaye anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful - Sudan. Hafla ya uvalishaji cheo imefanyika leo Novemba 18, 2013 katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
   Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( kulia) akimpongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge mara baada ya kumvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt.  Deus Clement Marenge ni miongoni mwa Maafisa wa Jeshi la Magereza ambao wanahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful - Sudan.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa nasaha fupi mara baada ya zoezi la uvalishaji cheo kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge( hayupo pichani) ambaye kwa sasa anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful - Sudan.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimpongeza Dkt. Deus Clement Marenge(wa tatu kulia) kwa kutosi vinywaji kama inavyoonekna katika picha mara baada ya hafla fupi ya uvishaji cheo kwa Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza ambaye amevishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kamishna wa Magereza wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(aliyesimama) akimpongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge mara baada ya zoezi la uvalishaji cheo lililofanyika leo Novemba 18, 2013 katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

Comments