WAAJIRI WAASWA KUTOA SEMINA ELEKEZI KWA WAFANYAKAZI KABLA YA KUSTAAFU


IMG_9057
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maazimo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa 23 wa wanachama na wadau wa mfuko huo uliofanyika Arusha October mwaka huu ambapo moja ya maazimio ni waajiri kuwapa fursa wafanyakazi wao kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii.katikati ni Meneja Uwekezaji wa mfuko huo Bw. Selestine Some na Mwishoni ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi. Fatma Salum.IMG_9082Meneja Huduma kwa Wateja na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. Godfrey Mollel akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mpango wa mfuko huo kufikisha wanachama 400,000 ifikapo mwaka 2015, kwa sasa mfuko huo una wanachama takribani 300,000,kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele.IMG_6099Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Hassan Silayo- MAELEZO
Na Hassan Silayo-Maelezo
Waajiri nchini wametakiwa kuwa utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi anapoingia katika ajira.
Wito huo umetolewa na meneja uhusiano na masoko wa mfuko wa pensheni wa PPF Lulu mengele wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini dar es salaam. 
Megele alisema kuwa kumekuwa na tabia ya waajiriwa kusahau kujiwekea akiba na hivyo kusababisha matatizo wakati wa kustaafu.
”napenda kuwaasa waajiri waanzishe utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi anapoingia katika ajira hii itamsaidia mfanyakazi kuwa na mipango ya maandalizi kabla ya kustaafu na sio kusubiri mtu astaafu ndio aanze kuweka mipango ya maisha yake”. Alisema Mengele.
Pia Menegele aliongeza kuwa kuna haja ya waajiri nchini kuwapa fursa Wafanyakazi wapya kujiunga na Mifuko mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii.
“napenda kuwaasa waajiri wote nchini kuwapa fursa wafanayakazi wapya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kwa kufanya hivi kutaweza kuwasaidia wafanyakazi kuwa na uwezo wa kujikimu na kukabiliana na changamoto za maisha katika siku za baadae” alisema Mengele. 
Akieleza mipango ya kuongeza wanachama meneja wa huduma kwa wateja na wanachana Godfrey Mollel alisema wanamipango ya kuongeza wanachama hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2015. 
“kwasasa tuna wanachama 300,000 lakini kutokana na ubora wa huduma za PPF tunategemea kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2015.
Mfuko wa pensheni wa PPF unajivunia kutekeleza majukumu yake kwa asilimia 80 kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mwasiliano(TEHAMA).

Comments