Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(katikati)akiwaonesha moja ya namba ya simu ya mshindi aliejishindia Pikipiki katika promosheni ya”Timka na Bodaboda” kwa Ofisa wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid(Kushoto)na Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Emmanuel Ndaki.Wakati wakichezesha droo ya promosheni hiyo,jumla ya washindi(125)wamejishindia Pikipiki na fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni (70)zimenyakuliwa.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544.
Timka na Bodaboda ya Vodacom yafikia patamu
Bodaboda 125 na Milioni 70 tayari zimenyakuliwa
Dar es Salaam,Huku maisha ya maelfu ya Watanzania yakiendelea kuboreshwa siku hadi siku kupitia Promosheni ya “Timka na Boda Boda” inayoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania. Jumla ya Watanzania 125 wamejishindia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda na milioni fedha taslimu Milioni 70 zikinyakuliwa.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, amesema siku zote Vodacom imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaboresha maisha ya wateja wake ambao mchango wao umeifanya kampuni hiyo kuendelea kuwa namba moja hapa nchini.
“Lengo letu sisi kama Vodacom ni kuhakikisha tunaendelea kuimarisha maisha ya wateja wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono siku zote, Tunaamini kuwa kwa kuboresha maisha ya wateja wetu kutoka katika faida tunayoipata ili kuwawezesha wao kuendelea pia kutuunga mkono siku hadi siku na kwa nguvu zaidi,” alisema Nkurlu na kuongeza
No comments:
Post a Comment